Genesis 17:2-7

2 aNami nitafanya Agano langu kati yangu na wewe, nami nitakuzidisha sana sana.”

3 bAbramu akaanguka kifudifudi, naye Mungu akamwambia, 4 c“Kwa upande wangu, hili ndilo Agano langu na wewe: Wewe utakuwa baba wa mataifa mengi. 5 dJina lako hutaitwa tena Abramu, bali jina lako litakuwa Ibrahimu,
Ibrahimu maana yake Baba wa watu wengi.
kwa maana nimekufanya wewe baba wa mataifa mengi.
6 fNitakufanya uwe na uzao mwingi sana, kwako yatatoka mataifa nao wafalme watatoka kwako. 7 gNitalithibitisha Agano langu kama Agano la milele kati yangu na wewe na wazao wako baada yako na vizazi vijavyo niwe Mungu wako na Mungu wa wazao wako.
Copyright information for SwhKC